EWURA Banner
HabariLeo Logo
 
Tafuta:
 
HABARI KATIKA PICHA
 
Wafanyakazi wa Kampuni ya MEES wakiweka nguzo ya umeme katika eneo la Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship lililopo barabara ya Sam Nujoma Dar  es Salaam jana. (Na Mpigapicha Wetu).

Imetayarishwa na:
Imewekwa tarehe: 9th March 2010 @ 18:12
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi(CUF), Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya Hindu Mandal,Dar es Salaam alikolazwa kwa matibabu.Taarifa kutoka kwa madaktari wanaomhudumia zinasema anasumbuliwa na shinikizo la damu na kwa sasa hali yake inaendelea vizuri(Mpigapicha Wetu)

Imewekwa tarehe: 9th March 2010 @ 09:40
 
Imetayarishwa na:
Imewekwa tarehe: 8th March 2010 @ 19:37
 
MWANA UMLEAVYO...Mtoto mdogo anayeelelewa katika makazi ya Kulea Watoto Yatima na wasio na Makazi Maalum wa CHAKUWAMA kilichopo Sinza Dar es Salaam akiwa amemuwekea sanamu ya bastola mwenzake wakati wanacheza. Wazazi na walezi wanaopaswa kuangalia vitu vya kuwanunulia watoto kuchezea wakiwa wadogo kwani wanaweza kuona silaha halisi ndani na kufyatulia watu akidhani kuwa ni toi. (Picha na Mroki Mroki).

Imewekwa tarehe: 7th March 2010 @ 17:32
 
'Ngoja ni hakikishe'
'Ngoja ni hakikishe'
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe akihakiki vipimo vilivyoko karika mchoro wa mradi wa umeme unaotakiwa kupita katika eneo la kanisa hilo, Mwenge, Dar es Salaam. Mradi huo ulizua utata miezi miwili iliyopita na sasa muafaka unaelekea kupatikana. (Picha na Gloria Tesha)

Imewekwa tarehe: 6th March 2010 @ 19:16
 
Mke wa aliyekua Jaji Mkuu wa kwanza hayati Augustine Saidi, Elizabeth Kilasara (kushoto) na Mke wa Jaji Mkuu Augustino Ramadhani, Sada Ramadhani wakiangalia sanamu ya hayati Saidi baada ya kuifunua. Wakati wa sherehe ya Uzinduzi wa Jengo la Ukumbusho wa  Jaji huyo. (Na Mpigapicha Wetu).

Imewekwa tarehe: 5th March 2010 @ 17:26
 
Rais Jakaya Kikwete akijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura katika kituo kipya cha kupigia kura kijijini kwake Msoga,Wilayani Bagamoyo jana.Pembeni ni msimamizi wa kituo Diana Fredrick,  zamani  Rais alikuwa akipiga kura katika kituo cha Bwilingu, Kata ya Chalinze, wilayani humo. (Picha na  Freddy Maro).

Imewekwa tarehe: 4th March 2010 @ 18:00
 
Wakazi wa kijiji cha Mihima kilichoko katika kata ya Nyamupa Lindi vijijini wakiendelea na shughuli ya kujenga barabara inayoelekea kijijini humo.Tangu Tanzania ipate  uhuru kijiji hicho kilikuwa hakina mawasiliano ya barabara hadi Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)ulipotekeleza mradi  wa kujenga barabara hiyo yenye urefu karibu kilometa saba. (Picha na Lucy Lyatuu)

Imewekwa tarehe: 3rd March 2010 @ 18:09
 
Maji taka na uchafu ulio ndani ya ukuta wa majengo ya kituo cha Polisi cha Msimbazi unatishia afya za wakazi wa eneo hilo kama ulivyonaswa na kamera ya mpiga picha wetu Kariakoo jijini Dar es Salaam jana. Hatua za dharura zinapaswa kuchukuliwa kuepusha magonjwa ya kuhara na kipindupindu. (Picha na Robert Okanda)

Imewekwa tarehe: 2nd March 2010 @ 17:17
 
Ndege ya ATCL aina ya Boeing 737 ikiwa imelalia tumbo baada ya tairi lake la mbele kupasuka jana asubuhi wakati ikitua katika uwanja wa ndege wa Mwanza. Hakuna majeruhi katika ajali hiyo.(Na Mpigapicha Wetu).

Imewekwa tarehe: 1st March 2010 @ 18:35
 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtanda katika mkoa wa Lindi na mkazi wa eneo hilo wakichota maji katika kisima kilichojengwa kwa msaada wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini (TASAF).(Picha na Fadhili Akida)

Imewekwa tarehe: 1st March 2010 @ 07:38
 
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Seif Shariff Hamad wakati wa mazishi ya mwanasiasa mkongwe na mwanadiplomasia marehemu Balozi Daudi Mwakawago, yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana jioni.

Imewekwa tarehe: 27th February 2010 @ 18:28
 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akimkabidhi  Mtendaji  wa Kata ya Urambo  Mjini, Stella  Riwa Pikipiki  ili aweze kufanya kazi yake  vizuri.Kushoto ni mke wa Pinda,Tunu na watatu kushoto ni Spika wa Bunge la Tanzania, Mbunge wa Urambo, Samuel Sitta. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Imewekwa tarehe: 27th February 2010 @ 07:42
 
Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia viongozi waandamizi wa TAKUKURU wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa taasisi hiyo mjini Mwanza  jana. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa TAKUKURU Dk. Edward Hosea na kushoto ni Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Sofia Simba. (Picha na Freddy Maro).

Imewekwa tarehe: 25th February 2010 @ 17:51
 
Mhitimu wa masomo ya  Kidato cha sita kutoka  Shule ya Sekondari ya Lutheran Junior Seminary  ya Morogoro,  Ninoo Palanda  wa (katikati) wa Jamii ya wafugaji wa Kimasai,  Kijiji cha Wami Sokoine akiwa na ndugu zake wakati wa Sherehe ya Mahafali ya 39 ya Kidato cha sita ya shule hiyo yaliyofanyika juzi. (Picha zote na John Nditi).

Imewekwa tarehe: 24th February 2010 @ 16:59
 
Meli ya kivita ya Marekani, USS Farragut, iliyoshiriki kuiokoa meli ya MV Barakaale 1 ilipovamiwa na maharamia wa kisomali katika ghuba ya Aden Jumapili iliyopita. (Picha ya Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania).

Imewekwa tarehe: 24th February 2010 @ 10:41
 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na mkewe, Tunu wakiwasalimia  wananchi  wa Mji Mdogo wa Nzega mkoani Tabora baada ya kiongozi huyo wa Serikali kuhutubia  mkutano wa hadhara kwenye  viwanja  vya Parking  mjini hapo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Imewekwa tarehe: 23rd February 2010 @ 18:23
 
Mmoja wa wakazi wa Mbagala, Dar es Salaam, walioathiriwa na milipuko ya mabomu Aprili mwaka jana, Johari Ali (kushoto) akizungumza na wageni wake nje ya hema anapoishi. Mwananchi huyo anadai kuwa hajalipwa fidia, na imefahamika kwamba waathirika waliopewa mahema walitakiwa kuyarudisha kwenye mamlaka husika ili yakatumike katika maeneo mengine yaliyokumbwa na maafa. (Picha na Mroki Mroki).

Imewekwa tarehe: 22nd February 2010 @ 17:19
 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akipata  maelezo kuhusu  bwawa la maji la Mwamapuli wilayani Igunga, Tabora  kutoka  kwa Mbunge wa Jimbo hilo, Rostam Aziz (wa tatu kulia) wakati alipokagua bwawa hilo  linalotumika katika  kilimo cha  umwagiliaji. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimussa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Imewekwa tarehe: 22nd February 2010 @ 07:23
 
Rais Jakaya Kikwete akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa kutoka Chuo Kikuu cha Faith cha mjini Instabul Uturuki ambayo amekabiziwa na Mkurugezni wa Chuo hicho Prof. Shariff Ali mjini humo juzi. Shahada hiyo ni kutokana na mchango wake katika kuendeleza mahusiano ya kimataifa. (Picha an Freddy Maro).

Imewekwa tarehe: 20th February 2010 @ 18:42
 
Mbeba Mizigo wa katika soko la Ndizi Manzese akiwa amebeba gunia la Viazi kutoka katika gari  jana. Wafanyabiashara wameitikia wito wa kutojaza magunia ya viazi na nafaka lumbesa lakini bado wamedai kusumbuliwa sokoni hapo licha ya ujazo huo kubadilika. (Picha na Mroki Mroki).

Imewekwa tarehe: 19th February 2010 @ 17:55
 
Rais Jakaya Kikwete na mwenyeji wake, Rais wa Uturuki Abdukkah Gul, wakikagua gwaride la heshima muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuwasili katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Ankara jana asubuhi. (Picha na Freddy Maro)

Imewekwa tarehe: 18th February 2010 @ 17:55
 
Balozi wa Ufaransa nchini Jacques de Labriolle (kushoto) akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania, Alhaji Adam Kimbisa baada ya Ubalozi huo kukabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi Milioni 100 kwa ajili ya waathirika wa mafuriko Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro. Makabidhiano hayo yalifanyika jana Dar es salaam makao makuu ya Msalaba Mwekundu. (Picha na Mroki Mroki).

Imewekwa tarehe: 17th February 2010 @ 16:59
 
Mmoja wa Polisi wa Kikosi cha Reli Tanzania akijaribu kuwatuliza baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) waliofika katika ofisi za makao makuu ya TRL kushinikiza kupewa mishahara yao jana. (Picha na Mroki Mroki).

Imewekwa tarehe: 16th February 2010 @ 17:16
 
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao pia ni mawaziri wakuu wastaafu, kutoka kushoto, Cleopa Msuya, Frederick Sumaye, na Edward Lowassa wakiteta wakati wa kikao  cha halmashauri hiyo mjini Dodoma. (Picha na Freddy Maro)

Imewekwa tarehe: 15th February 2010 @ 18:09
 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania, Samuel Sitta, akisalimiana na wajumbe wenzake ambao pia ni mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye (Kushoto) na Edward Lowassa, kabla ya kuanza kwa mkutano wa NEC mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Imewekwa tarehe: 15th February 2010 @ 08:09
 
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete (wa tatu kulia) na viongozi waandamizi wa Kamati Kuu ya CCM wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka hayati Mzee Rashid Kawawa muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha kamati hiyo mjini Dodoma jana asubuhi. Kutoka kushoto Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, Rais Amani Abeid Karume, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na Makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa (Picha na Freddy Maro)

Imewekwa tarehe: 13th February 2010 @ 17:38
 
Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald akiongozwa na Polisi kuingia katika mahabusu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni Dar es Salalaam jana alikpofikishwa pamoja na rafiki yake Kennedy Victor kusomewa mashitaka ya kushambulia na kuharibu mali. Miriam alipelekwa mahabusu kwa kukosa mdhamini. (Picha na Mroki Mroki).

Imewekwa tarehe: 12th February 2010 @ 17:18
 
Baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wanaounda kikundi cha TANZIBAT 1 wakipaanda  kwenye ndege katika Uwanja wa Kimataifa wa  Mwalimu Julius Nyerere juzi tayari kwa safari ya kwenda kwenye ulinzi wa Amani katika jimbo la Darfur Nchini Sudan. Jumla ya askari wapatao 600 hadi leo watakuwa wameshaondoka kuungana na wengine katika jukumu la ulinzi ambapo wanatarijwa kufanyakazi kwa kipindi cha mwaka mmoja. (Picha na Alex Malima wa JWTZ)

Imewekwa tarehe: 12th February 2010 @ 16:54
 
Mwanamuziki Nguza Viking, maarufu kwa jina la Babu Seya, akimfariji mwanawe, Papii Nguza, wakati Mahakama ya Rufaa Tanzania ilipotoa hukumu ya rufaa yao kwa kuamuru waendelee na kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kubaka na kulawiti watoto, Sinza, Dar es Salaam.( picna na Mroki Mroki).

Imewekwa tarehe: 12th February 2010 @ 11:14
 
Mwanamuziki Nguza Viking (kushoto) na wanawe, kutoka kushoto Papii Nguza, Nguza Mbangu, na Francis Nguza wakiwa katika Mahakama ya Rufani Tanzania, Dar es Salaam kusomewa hukumu ya rufaa yao kupinga adhabu ya kifungo cha maisha jela. Mbangu na Francis wameachiwa huru. (Picha na Mroki Mroki).

Imewekwa tarehe: 11th February 2010 @ 17:43
 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akizungumza na Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma. Mkutano wa 18 wa Bunge la Tanzania unaendelea mjini humo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Imewekwa tarehe: 10th February 2010 @ 17:39
 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akizungumza na Waziri Mkuu wa zamani, Mbunge  wa  Monduli, Edward  Lowassa, kwenye viwanja vya  Bunge mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Imewekwa tarehe: 9th February 2010 @ 17:57
 
Baadhi ya wauguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Temeke wakisaidia kumpakia kwenye gari la wagonjwa mmoja wa majeruhi wa ajali ya daladala kugonga treni iliyotokea eneo la Davis Kona, Yombo Dar es Salaam jana. (Picha na Fadhili Akida).

Imewekwa tarehe: 8th February 2010 @ 17:21
 
Rais Jakaya Kikwete akikagua kingo za mto Mkondoa uliofurika na kuleta hasara kubwa ya mali katika mji wa Kilosa wakati alipotembelea wilaya hiyo ya Mkoa wa Morogoro jana kujionea na kuwajulia hali waathirika wa mafuriko yaliyotokea Desemba mwaka jana na mapema Januari mwaka huu. (Picha na Freddy Maro).

Imewekwa tarehe: 7th February 2010 @ 20:19
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Jakaya Kikwete (Wa pili kushoto mstari wa mbele) akiwasalimu wananchi (hawapo pichani) wakati wa matembezi ya mshikamano ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 33 tangu kuanzishwa kwa CCM. Kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho(Bara), Pius Msekwa, kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na mke wa Kikwete, Salma.(Picha a Fadhili Akida).

Imewekwa tarehe: 7th February 2010 @ 09:01
 
Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Jerry Muro (kulia) akiwa na ndugu yake wakitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. Muro na wenzake wawili wamesomewa mashitaka ya kuomba rushwa ya sh milioni 10. (Picha na Mpigapicha wetu).

Imewekwa tarehe: 5th February 2010 @ 17:44
 
Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akisalimiana na mmoja wa waasisi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chausiku Mussa (75) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika katika eneo la Mahakama Kuu, Dar es Salaam jana. Kushoto kwa Rais ni Spika wa Bunge la Tanzania, Samuel Sitta. (Picha na Fadhili Akida).

Imewekwa tarehe: 4th February 2010 @ 23:59
 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, akiwa kwenye foleni ya chakula cha mchana na askari walioko kambi ya muda Msata mkoani Pwani, wanaojiandaa kwenda Sudan kwenye ulinzi wa amani, alipowatembelea juzi. (Picha kwa hisani ya JWTZ).

Imewekwa tarehe: 3rd February 2010 @ 18:50
 
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akiwatambulishwa watuhumiwa wa utapeli Edmunda Kapama (kushoto) na Deogratius Ngassa kwa wanahabari jana katika Kituo Kikuu cha Polisi,akiwahusisha katika tuhuma za kutoa vitisho na kuomba rushwa zinazomkabili mwandishi wa habari, Jerry Muro.(Picha na Muhidin Michuzi)

Imewekwa tarehe: 3rd February 2010 @ 08:57
 
Imewekwa tarehe: 2nd February 2010 @ 23:59
 
Rais Jakaya Kikwete (kulia) akisalimiana na Rais wa
Jamhuri ya Libya, Muammar Gaddafi wakati wa kikao cha 14 cha wakuu wa nchi za Afrika kinachofanyika  Addis Ababa nchini Ethiopia kilichoanza juzi nakutarajiwa kumalizika leo.
Katikati ni Rais Omar el Bashir wa Sudan. (Picha na John Lukuwi wa Maelezo).
Rais Jakaya Kikwete (kulia) akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Libya, Muammar Gaddafi wakati wa kikao cha 14 cha wakuu wa nchi za Afrika kinachofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia kilichoanza juzi nakutarajiwa kumalizika leo. Katikati ni Rais Omar el Bashir wa Sudan. (Picha na John Lukuwi wa Maelezo).
Imetayarishwa na:
Imewekwa tarehe: 1st February 2010 @ 19:37
 
Imetayarishwa na:
Imewekwa tarehe: 1st February 2010 @ 19:00
 
Mume wa marehemu Jacqueline Minja, Deo Minja (kushoto) akisadiana na watoto wake Debra (katika) na Dudley (kulia) kuweka shada la maua katika kaburi la mama yao mara baada mazishi yaliyofanyika katika kijiji cha Rauya-Marangu mkoani Kilimanjaro.Jacqueline aliuawa kwa kupigwa risasi na majambazi Januari 26 mjini Arusha.(Picha na Paul Sarwatt).

Imewekwa tarehe: 31st January 2010 @ 18:44
 
Shule nyingi za msingi vijijini bado hazina majengo imara na salama kwa kusomea watoto kama hili la Shule ya Msingi Mlamleni iliyopo Wilayani Mkuranga mkoani Pwani. Jengo hilo la madarasa mawili lipo hatarini kuangakuka na shule inakabiliwa na uhaba wa madarasa. (Picha na Mroki Mroki).

Imewekwa tarehe: 30th January 2010 @ 17:39
 
Rais Jkaya Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais wa zamani wa Marekani, Bill Cliton mjini Davos, Uswisi jana ambapo wawili hao wanahudhuria kongamano la kiuchumi la Duniani(Picha  na Freddy Maro)

Imewekwa tarehe: 28th January 2010 @ 20:15
 
Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mtoto wa Chifu Fundikira, ambao ni askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Koplo Ali Ngumbe(Kushoto) na Sajini Rhoda Robert wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Dar es Salaam kusomewa mashtaka yao  jana.

Imetayarishwa na: Fadhili Akida
Imewekwa tarehe: 27th January 2010 @ 20:08
 
Makamu wa Rais   Dk Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Kenya, Mwai Kibaki, wakati alipotembelea ofisini kwake Harambee House mjini Nairobi,Kenya jana, Makamu wa Rais yupo Kenya kwa ziara tya Kiserikali ya siku tatu

Imetayarishwa na: Amour Nassor
Imewekwa tarehe: 26th January 2010 @ 20:08
 
Mkurugenzi wa tume ya Taifa ya uchaguzi(Nec), Rajabu Kiravu(kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu taratibu za ugawaji wa majimbo ya uchaguzi wa Bunge unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, Dar es salaam jana. Mwingine ni makamu mwenyekiti wa tume hiyo, Omar Makungu.(Picha na Fadhili Akida)

Imewekwa tarehe: 26th January 2010 @ 00:35
 
Wasiliana nasi mhariri@habarileo.co.tz, advertising@dailynews.co.tz
Simu:+255 22 2 127492 au 22 2 116074 au +255 22 2 110595 au 22 2 127493
HabariLeo © 2009 Haki zote zimehifadhiwa.
DailyNews Building, Plot 7, Samora Avenue, Box 9033, Dar es Salaam, Tanzania Copyright © 2009 DailyNews Media Group
Advertisement
TSN Adveritising