Ukaguzi gerezani

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (kushoto) akiongozwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mtwara (RPO), Ismail Mlawa (kulia) kuingia gereza la Kilimo na Mifugo Namajani lililopo wilayani Masasi kwa ajili ya ukaguzi akiwa katika ziara ya mkoa huo mwishoni mwa wiki. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

Add a comment

Picha ya pamoja

Rais John Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakiwa katika picha na maofisa walioapishwa Ikulu Dar es Salaam. Maofisa walioapishwa ni Jaji Stella Mugasha ambaye anakuwa Kamishna wa Tume ya Mahakama, Sylvester Mabumba (Balozi wa Tanzania nchini Oman), Job Masima (Balozi wa Tanzania nchini Israel), Dk Abdallah Possi (Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani), Profesa Palamagamba Kabudi (Waziri wa Sheria na Katiba) na Dk Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.(Picha na Ikulu).

Add a comment

Tatizo sugu

Tatizo la maji safi bado limekuwa sugu kwa vijiji vingi vya Mkata wilayani Handeni, Tanga. Pichani, madumu ya maji yakiwa yamepangwa kandokando ya barabara kuu ya Chalinze-Segera eneo la Mkata yakisubiri kujazwa maji safi. (Na Mpigapicha Wetu).

Add a comment