MAZIKO - ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) akijumuika na viongozi mbalimbali na Waislamu katika maziko ya aliyewahi kuwa Waziri katika Serikali hiyo, Mzee Taimur Saleh Juma katika makaburi ya Kianga Wilaya ya Magharibi “A” Unguja juzi. (Picha na Ikulu).

Add a comment

TREKTA - KUTAZAMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama moja kati ya matrekta aina ya Ursus yanayounganishwa kwenye karakana ya Tamco mjini Kibaha mkoani Pwani juzi, alipotembelea kiwanda hicho. Kulia kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Add a comment

KUKATA UTEPE

Mkuu wa wilaya Kigoma, Samson Anga (wa pili kulia) na Spika Mstaafu, Anne Makinda ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa utoaji huduma kupitia mpango wa madaktari bingwa wanaotembea utakaofanyika mkoani Kigoma kwa wiki moja kwa udhamini wa mfuko huo.

Add a comment

AKIHUTUBIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mimi na Wewe uliofanyika kwenye uwanja wa Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge, mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.

Add a comment

JIM AKIFURAHI NA WILSON JACKSON

Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Serikali ya Daily News, HabariLeo na SpotiLeo, Dk Jim Yonazi akifurahi na Wilson Jackson (13) aliyekuja na mama yake, Neema Ndossi (wa pili kushoto) katika ofisi za TSN Dar es Salaam jana, kutoa shukrani kufuatia magazeti hayo kuchapisha habari zilizomsaidia kupata msaada wa fedha za matibabu kutoka kwa jamii, baada ya mtoto huyo kugongwa na lori na kuumia ubongo na miguu. Kushoto ni mkwe wa mama huyo anayemsaidia malezi, Alex Silago.

Add a comment

MV KAZI

Abiria wakiingia katika kivuko kipya cha MV Kazi kabla ya kuvuka kwa mara ya kwanza kutoka Magogoni kwenda Kigamboni jijini Dar es Salaam jana baada ya kukamilika ujenzi wake hivi karibuni. Kivuko hicho cha tani 170 kimejengwa kwa thamani ya Sh 7.3 bilioni.

Add a comment