KUBADILISHANA MAWAZO

Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack wakati wa semina ya Jukwaa la Biashara lililofanyika mkoani humo jana kwa uratibu wa kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN). Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe. (Picha na Katuma Masamba).

Add a comment

KUKATA UTEPE

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Salum Kijuu (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi jipya la NMB Kaitaba lililopo Manispaa ya Bukoba ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Protase Tehingisa pamoja na Kaimu Ofisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati, Abdulmajid Nsekela wakishuhudia uzinduzi huo. (Na Mpigapicha Wetu).

Add a comment

KUSALIMIANA

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilayani Monduli, Loota Sanare (katikati) akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa chama hicho jana kabla ya uchaguzi wa nafasi mbalimbali (Picha na Veronica Mheta).

Add a comment

SALAMU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mwenezi Msaidizi wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Johari Yusuf, baada ya ufunguzi wa mkutano wa chama hicho mjini Lindi jana. Katikati ni Rais wa Chama hicho, Poul Magesa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Sebastian Luziga (kulia).

Add a comment

KUONESHA

Ofisa anayeshughulikia utamaduni katika Ubalozi wa Marekani nchini, Jeff Ladenson (kushoto) akimuonesha Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Stella Manyanya umbo la ramani ya Tanzania lililotengenezwa na mashine maalumu ya “3D Printer” katika kituo kipya cha Kimarekani wakati wa uzinduzi wa kituo hicho kilichopo katika Maktaba Kuu ya Taifa hivi karibuni. Anayeshuhudia ni Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Dk Inmi Patterson. (Picha kwa hisani ya Ubalozi wa Marekani).

Add a comment

MSISITIZO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisisitiza jambo wakati alipotembelea hospitali ya Temeke kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kitengo cha wagonjwa wa huduma ya haraka na dharura uliofadhiliwa na Ubalozi wa Japan nchini jana. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva (kulia), Mganga Mkuu wa Temeke, Dk Gwamaka Mwabulambo (wa pili kushoto), Mganga Mfawidhi, Amaan Malima na viongozi wengine. (Picha na Badi Yusuf).

Add a comment