Kupongezana

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk Hassan Abbas (kushoto) akimpongeza Kaimu Mhariri wa gazeti la Habarileo, Nicodemus Ikonko baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT) katika Mahafali ya 18 yaliyofanyika mjini Mwanza, jana. Dk Hassan Abbas alitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Mawasiliano ya Umma ya chuo hicho. (Picha na Nashon Kennedy).

Add a comment

Mali za chama

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rodrick Mpogolo (wa pili kulia) akikagua moja ya magari ya chama hicho wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa mali za chama mjini Dodoma. (Picha na Bashir Nkoromo).

Add a comment

Kutenga maeneo

Kutokana na migogoro ya mara kwa mara ya wakulima na wafugaji, Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero imeanza utaratibu wa kutenga maeneo maalumu ya makazi, mifugo na kilimo kama kinavyoonesha kibao cha makazi ya wananchi wa Kijiji cha Mafuta, Kata ya Muhonda wilayani humo kikitoa maelekezo kwa wananchi hao. (Na Mpigapicha Wetu).

Add a comment

Mtoto kupooza

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amkisikiliza baba wa mtoto Alex Andrea aliyepooza viungo vya mwili, akielezea madhila anayoyapata baada ya mke wake kumkimbia wakati mtoto huyo akiwa na umri wa miaka 3 baada ya kugundua amepooza. Mzazi wa mtoto huyo alifika ofisini kwa Makonda kuomba msaada wa matibabu na matunzo ya mwanae ambapo Makonda aliahidi kumsaidia Sh milioni moja kila mwezi mtoto huyo. (Picha na Yusuf Badi).

Add a comment

Heshima za mwisho

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, marehemu Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki aliyefariki juzi katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi JWTZ Lugalo Dar es Salaam, baada ya kuugua kwa muda mfupi. ([Picha na Ikulu).

Add a comment