Wajane wa Sokoine

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Napono Sokoine na Nekiteto Sokoine (kulia) ambao ni wajane wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Sokoine wakati aipokwenda nyumbani kwao, Monduli Juu kuisalimia familia akiwa katika ziara ya wilaya ya Monduli jana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Add a comment

Wanafunzi UDSM

Meneja Masoko wa Benki ya Barclays Tanzania, Joe Bendera (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) jijini mwishoni mwa wiki katika mkutano ambao benki hiyo iliitambulisha programu yake ya ‘Read to Work’ yenye lengo la kuwaandaa wahitimu wa vyuo vikuu na elimu ya juu kujiandaa na ajira au kujiajiri. (Na Mpigapicha Wetu).

Add a comment

Mhitimu pekee

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mkuu mstaafu, Barnabas Samatta akimtunuku Shahada ya Udaktari wa Falsafa mhitimu pekee kwa mwaka huu, Ismail Juma Ismail ambaye ni mlemavu wa viungo wakati wa mahafali ya 15 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Kampasi Kuu ya Mzumbe, Morogoro. (Picha na John Nditi).

Add a comment

Kofia ngumu

Mwendesha pikipiki akipita katika eneo la Michenzani Mjini Unguja akiwa amepakia abiria bila kuvaa kofia ngumu, jambo ambalo ni hatari na ni kinyume cha Sheria za Usalama Barabarani. (Picha na Mroki Mroki).

Add a comment

Kitabu cha maombolezo

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha maombelezo ya aliyekuwa Rais wa Cuba na mwanamapinduzi mashuhuri duniani, Fidel Castro aliyefariki dunia Novemba 25, mwaka huu jijini Havana, Cuba. Kushoto ni Balozi wa Cuba nchini, Balozi Jorge Luis Lopez Tormo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Add a comment

Majora ya vitenge

Naibu Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Nguo cha Urafiki, Shadrack Nkelebe (wa pili kulia) akikabidhi sehemu ya majora ya vitenge kwa fundi mahiri wa nguo ambaye hata hivyo ni mlemavu wa macho, Abdallah Nyangalio (kushoto) katika hafla fupi iliyofanyika Dar es Salaam, jana. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva (katikati) na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka. (Pichana Yusuf Badi).

Add a comment