AKIKAGUA VIFAA TIBA

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akikagua vifaa tiba vya wajawazito baada ya kukabidhiwa na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem, Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Add a comment

WAKIONESHA UMAHIRI

Askari wapya wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kundi la 37 la mwaka 2016 waliokuwa wakipatiwa mafunzo kwa wiki 18 katika Shule ya Mafunzo ya awali ya kijeshi (RTS Kihangaiko) mkoani Pwani, wakionesha umahiri na ukakamavu kwa kupitiwa juu na pikipiki wakati wa ufungaji wa mafunzo yao katika Uwanja wa Jeshi la Kujenga Taifa Oljoro 833KJ Arusha.

Add a comment

WAKIMSIHI ASIVUNJIKE MOYO

Mbunge wa Urambo Mashariki, Margareth Sitta (CCM) na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde wakimsihi Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mollel (CCM) asivunjike moyo baada ya kushindwa kuwasilisha hoja binafsi bungeni Dodoma.

Add a comment

AKISISITIZA JAMBO

Naibu Mwanasheria wa Serikali, Gerson Mdemu akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake wa kazi na watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mkoani Tabora wakati wa Wiki ya Utumishi wa Umma. Kushoto kwake ni Wakili wa Serikali Mfawidhi, Jackson Bulashi na Mkurugenzi wa Utumishi na Rasilimali Watu, Benny Kabungo.

Add a comment

MAHAKAMANI

Harbinder Singh (kulia) na James Rugemarila (kulia kwake) wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam walipofikishwa kujibu mashitaka ya uhujumu uchumi.

Add a comment