Kukabidhi msaada

Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Guido Kayuki (kulia) akikabidhi msaada wa madawati 12, vioo 234 na mifuko 64 ya saruji kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Amelchiory Kulwizila, vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh milioni 2.4. Msaada huo ulitolewa kwa ajili ya Shule ya Msingi Lupeta. (Picha na Joachim Nyambo).

Add a comment

Kuzindua kisima

Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Charles Kuyeko (kulia) akizindua kisima katika shule ya Msingi Kifuru Tabata chenye thamani ya Sh milioni 28 kilichojengwa kwa msaada kutoka Afirica Muslims Agency ya Kuwait. Katikati ni Mkurugenzi msaidizi wa Africa Muslims Agency, Mahmoud Idris. (Na Mpigapicha Wetu).

Add a comment

Kikao kazi

Washiriki wa kikao kazi cha mafunzo ya utambulisho wa miongozo mikuu ya Mfumo wa Kuzipitia Ruzuku ya Maendeleo Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGDG) wakiwemo wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya, miji, manispaa na majiji pamoja na maofisa mipango, utumishi, maendeleo ya jamii na wahazini kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Dodoma na Morogoro, wakiwa katika mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoanza mjini Dodoma yakilenga kuwajengea uwezo wa namna ya kuboresha matumizi ya ruzuku isiyo na masharti. (Picha na John Nditi).

Add a comment

Kumenya viazi

Akinamama wa Kikundi cha 2Seeds cha Kijiji cha Tabora Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wakishirikiana na Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald (wa pili kushoto) kumenya viazi wakati alipotembelea kikundi hicho hivi karibuni kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ya ujasiriamali, ufugaji na kilimo inayofanywa na kikundi hicho na kufadhiliwa na Mfuko wa Kusaidia Jamii wa Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la 2Seeds Network la Marekani. (Picha kwa hisani ya Vodacom).

Add a comment