UTAFITI

Mtafiti mshiriki wa kukabiliana na sumu kuvu kwa njia ya kibaiolojia katika taasisi ya Kimataifa ya Kilimo cha Kitropiki (IITA), Jacob Njela akifafanua masuala ya kitafiti kuhusu sumu kuvu kwa waandishi wa habari wakati walipotembelea maabara ya taasisi hiyo iliyopo Mikocheni, Dar es salaam mwishoni mwa wiki. (Na Mpigapicha Wetu).

Add a comment

MKUTANO - DCPC

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo (katikati) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) ulioanza jana, Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa DCPC, Jane Mihanji na Kulia ni Makamu wake, Shadrack Sagati. (Picha na Mroki Mroki).

Add a comment

MAZUNGUMZO

Rais John Magufuli akizungumza na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) wakati alipokutana na viongozi hao Ikulu, Dar es Salaam jana. (Picha na Ikulu).

Add a comment

SHUKURANI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko (mwenye koti) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kumshukuru mfanyabiashara Azim Dewji (kushoto) kwa juhudi zake za kuwaleta wateja watakaopitisha mizigo yao bandari ya Dar es Salaam. Kushoto kwa Dewji ni Mkurugenzi wa Kampuni ya M.M. Integrate Steel ambaye pia ni wakala wa mizigo, Ratisn Kamania. (Picha na Yusuf Badi).

Add a comment

SALAMU

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akisalimiana na Mbunge wa Kuteuliwa, Salma Kikwete wakati wakiwasili bungeni mjini Dodoma juzi kuhudhuria vikao. (Picha na Mohamed Mambo).

Add a comment

KUSIKILIZA

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah na Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (kushoto) wakimsikiliza Mbunge wa Viti Maalumu, Dk Immaculate Semesi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Add a comment