AKIFUNGUA JENGO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein alipokuwa akifungua jengo la madarasa 3 mapya katika shule ya Kijitoupelele akiwa katika ziara yake ya kutembelea maendeleo ya Miradi ya maendeleo Wilaya ya Magharibi ‘B’ katika Mkoa wa Mjini Magharibi.

Add a comment

AKIZUNGUMZA NA WANAFUNZI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wanafunzi wanaosomea fani ya udaktari jijini Havana nchini Cuba, jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi Cuba, Goodchance Tarimo na kulia ni Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Canada na Cuba, Leonce Bilauri.

Add a comment

AKITOA MAAGIZO

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Seleman Jafo akitoa maagizo kwa watendaji wa Halmashauri ya Chamwino, wakati wa kukagua mradi wa maji katika Kijiji cha Itiso Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino hivi karibuni.

Add a comment

UKAAJI MBAYA

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Saimon Haule akionesha ukaaji mbaya wa abiria katika bodaboda wakati wa mafunzo ya usalama barabarani. Katika mafunzo hayo alisema kwamba ukaaji huo ni wenye utata mkubwa na husababisha ajali.

Add a comment