Kuchambua dagaa

Wanawake wa jijini Mwanza wakichambua dagaa katika Soko la Samaki Mwaloni, Mwanza. Ujenzi wa viwanda vya dagaa ni moja ya maeneo yaliyo na fursa ya uwekezaji ambayo yatajadiliwa katika Jukwaa la Biashara lililoandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Aprili 11 mwaka huu. (Picha na Mroki Mroki).

Add a comment

Kusalimiana na masista

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na masista alipoungana na waumini, ndugu, jamaa na marafiki kumuaga Paroko Stephano Kaombwe, aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke. (Picha na Ikulu).

Add a comment