VYETI

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Two Hands ya Dar es Salaam, Lulu Naji (katikati) akiwapa vyeti vya ushiriki wa semina Mkurugenzi wa Kampuni ya Benbros Motors Ltd, Moufar Eshaq (kulia) na Meneja Biashara wa Kampuni ya Sytemax (T) Ltd, Jeannette Chumila juzi. (Na Mpigapicha Wetu).

Add a comment

BIDHAA - KUTAZAMA

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, William Makufwe (aliyeshika kikapu) na katibu Tawala Wilaya hiyo, John Mahali (kulia kwake) wakitazama bidhaa zinazotengenezwa na kikundi cha tupendane cha Segera wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi. (Na Mpigapicha Maalumu).

Add a comment

KAMPENI - KUPANDA MITI

Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Rosemary Senyamule akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mferejini kilichopo katika Kata ya Ruvu wilayani humo kuhusu kampeni iliyopamba moto ya upandaji miti ambapo kingo za mto Pangani ni miongoni mwa maeneo yaliyopandwa miti ikiwa ni mkakati wa kulinda na kuhifadhi mto huo. (Na Mpigapicha Wetu).

Add a comment

UFAFANUZI

Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa wafugaji kuhusu sheria sheria inayowazuia kuchunga mifugo kwenye maeneo yasiyoruhusiwa (Picha na Sifa Lubasi).

Add a comment