Mazao ya misitu

Mkuu wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Rehema Madusa akionesha mazao ya misitu zikiwemo mbao zilizokamatwa kwenye gari la Diwani wa Kata ya Kambikatoto kupitia Chama cha DemokrasianaMaendeleo (Chadema), Christopher Mchafu mjini humo. (Picha na Joachim Nyambo).

Add a comment

Barabara ya juu

Ujenzi wa barabara ya juu (flyover) katika makutano ya barabara za Mandela na Nyerere eneo la TAZARA jijini Dar es Salaam unazidi kushika kasi. Mafundi wa kampuni ya ujenzi ya Sumitomo Mitsui kutoka Japan tayari wameshasimamisha baadhi ya nguzo za daraja hilo. (Picha na Mroki Mroki).

Add a comment

Kusalimiana na wazee

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na mkewe Mama Mwanamwema wakisalimiana na wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati akirejea nchini kutoka Indonesia katika mkutano wa kwanza wa wakuu wa nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi alikomwakilisha Rais John Magufuli. (Picha na Ikulu).

Add a comment

Kusimama kwa muda

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres (kushoto) akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk Augustine Mahiga wakati Katibu Mkuu huyo aliposimama kwa muda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam. (Picha na Mroki Mroki).

Add a comment