Kumenya viazi

Akinamama wa Kikundi cha 2Seeds cha Kijiji cha Tabora Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wakishirikiana na Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald (wa pili kushoto) kumenya viazi wakati alipotembelea kikundi hicho hivi karibuni kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ya ujasiriamali, ufugaji na kilimo inayofanywa na kikundi hicho na kufadhiliwa na Mfuko wa Kusaidia Jamii wa Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la 2Seeds Network la Marekani. (Picha kwa hisani ya Vodacom).

Add a comment

Kuzindua ujenzi

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akizindua ujenzi wa jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi katika Kijiji cha Utengule wilayani Mbeya. Wanaoshuhudia ni baadhi ya mafundi wakiongozwa na Mhandisi wa Wilaya ya Mbeya, Jesse Shengena (kulia). (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

Add a comment

Kuvunja vibanda

Tingatinga la Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Pwani likivunja vibanda vilivyojengwa kwenye Soko la Maili Moja wilayani Kibaha mkoa ni humo kutokana na soko hilo kujengwa kwenye hifadhi ya barabara. (Picha na John Gagarini).

Add a comment

Rais kuhutubia

Rais Magufuli akihutubia baada ya hafla ya uwekaji saini mikataba mbalimbali kati ya Tanzania na Uturuki, Ikulu, Dar es Salaam. Kulia ni Rais wa Uturuki, Recep Erdogan.(Picha na Fadhili Akida).

Add a comment