Kubeba jeneza

Maofisa wa Polisi wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Kamanda wa Polisi wa zamani wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mohamed Chico wakati wa maziko yake yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam. Maziko hayo yaliongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu na kuhudhuriwa na wakuu wengine wastaafu wa jeshi hilo akiwemo Said Mwema, Omar Mahita, makamishna wastaafu na viongozi mbalimbali wa serikali. (Picha na Fadhili Akida).

Add a comment

Kuzungumza na wanafunzi

Kaimu Kamishna wa Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Nicholas Buretta akizungumza na wanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari Pugu katika maktaba yao mpya, iliyokarabatiwa na kuwekwa vitabu na kampuni ya Sahara Tanzania kwa kushirikiana na shirika la Read International, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano wa Sahara Group, Bethel Obioma. (Picha na Fadhili Akida).

Add a comment

Karibu Tanzania

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan aliyefuatana na mkewe, Emine Erdogan (kulia) wakifurahia ngoma kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam baada ya kuwasili kwa ziara rasmi nchini leo. Majaliwa alimpokea Rais huyo kwa niaba ya Rais John Magufuli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Add a comment

Kuvuka daraja

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), wakivuka kwenye daraja la kamba wakati wakielekea kukagua kampuni ya uzalishaji umeme wa maji katika eneo la Kikuletwa mkoani Kilimanjaro. Kampuni hiyo iliyojiondoa Tanesco kwa sasa imechukuliwa na Chuo cha Ufundi cha Arusha kinachofanyia mitambo yake matengenezo kwa ajili ya kuanza uzalishaji umeme. (Picha na Marc Nkwame).

Add a comment