KUIMBA

WAJUMBE wa Mkutano wa 19 wa mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), wakiimba wimbo wa jumuiya hiyo wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Dar es Salaam leo.

Add a comment

KUOKOA

Wananchi wakimuokoa dereva wa lori aina ya Fuso, Amir Mboriko baada ya kunusurika kifo yeye na utingo wake kufuatia lori alilokuwa akiendesha likiwa na shehena ya mchele kuacha njia na kupinduka katika mteremko wa Mapinduzi, Uyole mkoani Mbeya jana. (Picha na Mroki Mroki).

Add a comment

KUZUNGUMZA

Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Dk Stergomena Tax akizungumza wakati akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk Augustine Mahiga kufungua Mkutano wa 19 wa Mawaziri wa nchi za jumuiya hiyo, Dar es Salaam leo.

Add a comment

KUFARIJI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harison Mwakyembe pamoja na waombolezaji wengine wakimfariji Mke wa Spika wa zamani Samwel Sitta, Mama Magreth Sitta kutokana kupatwa na uchungu wakati wa kuaga na hatimaye maziko ya mke wa Dk Mwakyembe Linah Mwakyembe yaliyofanyika Wilayani Kyela mkoani Mbeya.

Add a comment

KUFUATILIA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), Spika wa Bunge Job Ndugai (Katikati) na Naibu Spika wa Bunge Dk Tulia Akson wakifuatilia shughuli za mazishi zinavyoenda nyumbani kwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk Harison Mwakyembe leo.

Add a comment