Wanariadha taifa kujipima Tigo Kili Marathon 2017

MASHINDANO ya Kilimanjaro Marathon yatafanyika mjini Moshi Februari 26, huku mbio za Tigo nusu marathon zikitarajia kuwa na msisimko wa aina yake.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabuday, mbio hizo za kilometa 21 zitakuwa na mvuti zaidi baada ya timu nzima ya taifa ya nyika ya Tanzania itashiriki mbio hizo.

Timu hiyo ya taifa itachaguliwa katika mashindano ya wazi ya mbio za nyika yatakayofanyika Moshi Februari 18 ikiwa ni siku chake kabla yam bio za Kili Marathon. Gida anasema kuwa, lengo la kuwashirikisha wanariadha hao wa timu ya taifa katika mbio za Tigo Marathon ni kuwawezesha wachezaji hao kujipima kwa uvumilivu wa mwili.

Wanariadha wa Taifa Wanariadha hao wa taifa watakuwa kambini West Kilimanjaro wakijiandaa kwa mbio za Dunia za Nyika zitakazofanyika Uganda Machi 26 mwaka huu na Tanzania inatarajia kupeleka timu kamili.

Gidabuday anasema kuwa kwa kuwa timu hiyo ya taifa itashiriki mbio za nyika, ambazo ni fupi kwa umbali, watashiriki Tigo Half Marathon ili kujipatia uvumivu wa mwili.

“Unajua mbio za nyika ni fupi, hivyo wanariadha wa timu ya taifa tutawashirikisha katika mbio za nusu marathon ili kuwaongezea uvulivu”,anasema. Tigo wenyewe wamejipanga Waandaaji wakishirikiana na Kampuni ya Tigo wamejipanga kuhakikisha mbio hizo zinakuwa na msisimko wa aina yake.

Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini wa Tigo, George Lugata anasema kuwa wameandaa zawadi za jumla ya Sh milioni 11 kwa ajili ya zawadi za washindi mwaka huu. Akifafanua kuhusu mgawanyo wa zawadi hizo, Lugata anasema kuwa, washindi wa kwanza kwa wanawake na wanaume katika mbio hizo za kilometa 21, ataondoka na kitita cha Sh milioni 2.

Anasema washindi wa pili kwa jinsi zote kila mmoja ataondoka na Sh milioni 1 huku washindi watatu kwa kila upande ataondoka na Sh 500,000. Lugata anasema kuwa wameandaa zawadi hadi kwa washindi wanne hadi wa 10 katika mbio hizo za kilometa 21.

Maboresho mengine Maboresho mengine yaliyofanyika mwaka huu ni pamoja na washiriki kuweza kujisajili kupitia mtandaoni na malipo kuyafanya katika mtandao wa Tigo Pesa. Lugata anasema kuwa hatua hiyo ya kujisajili kupitia mtandaoni kutasaidia kupunguza msongamano wa watu na malipo kuweza kufanyika kirahisi kabisa katika Tipo Pesa.

“Mwaka huu washiriki watajisajili kupitia mtandaoni na malipo watayafanya katika mtandao wa Tigo Pesa ili kuepusha msongamano, ambao hutokea kila mwaka, “anasema Lugata. Mbio za Kilimanjaro Marathon ni moja ya mbio kubwa zaidi kufanyika barani Afrika, ambapo zimekuwa zikishirikisha wanariadha wengi kutoka ndani na nje ya nchi.

Anasema kuwa mwaka mbio za kilometa 21 zitakuwa za aina yake kwa ubora kwani kila kitu kiko katika mpangilio. Mwaka huu wamejipanga zaidi Jamii inayozungumka mji wa Moshi imekuwa ikinufaika na mbio hizo na hasa kampuni ya tigo, ambayo imekuwa ikitoa fursa kibao kwa jamii kuanzia akina Mama Ntilie hadi wafanyabiashara wakubwa.