Rais mdogo zaidi duniani aliyeishia kunywa ‘mataputapu’

SIKU tatu baada ya kutimiza umri wa miaka 25 ya kuzaliwa, Valentine Strasser aliweka rekodi ya kuwa Rais mwenye umri mdogo kabisa duniani. Aprili 29, 1992, Strasser akiwa kijana mwanajeshi mwenye cheo cha kapteni, aliwaongoza wenzake kuvamia Ikulu ya Sierra Leone ambako walimkuta Rais Joseph Saidu Momoh akiwa amejificha ndani ya kabati lililopo bafuni, wakamteka na kumlazimisha kuikimbia nchi yake, naye bila kubisha akachukua helikopta na kutorokea Conakry, Guinea.

Add a comment