Choo kithaminiwe, kitunzwe

HIVI karibuni jumuiya ya Kimataifa imeadhimisha Siku ya Choo Duniani kwa lengo la kutoa fursa kwa viongozi, wataalamu wa afya na jamii kujadili juu ya madhara ya kiafya yanayotokana na matumizi duni ya choo. Siku ya Choo Duniani huadhimishwa Novemba 19 kila mwaka na hutumika kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa matumizi ya choo bora. Huhimiza wananchi kujiepusha na magonjwa mbalimbali yanayotokana na matumizi mabaya ya choo.

Add a comment