Wasomi wanamsaidiaje Rais Magufuli?

“TUNAISHI katika nchi ambayo mabinti wetu wadogo ambao wamefikia umri wa kuvunja ungo hawamudu kununua taulo za usafi, lakini wanawake na wanaume tulio nao katika ofisi zetu za umma, wana ‘ipads’ ambazo hata wengine hawajui namna ya kuzitumia.” Hiyo ni moja ya nukuu kati ya nukuu nyingi za Profesa Patrick Lumumba wa Kenya ambayo inapaswa, si tu kuandikwa kwa wino wa dhahabu, bali kumbadilisha mtazamo kila Mwafrika.


Add a comment

Soyinka alivyochana kadi ya ukazi kumpinga Trump

HIVI karibuni, vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa, vilikuwa na habari juu ya mshindi wa tuzo ya Nobel, Wole Soyinka kutimiza ahadi yake ya kuirarua kadi yake ya kijani inayompa kibali kuishi Marekani. 
Ahadi hiyo aliitoa wakati wa kipindi cha kampeni za uchaguzi wa rais nchini humo akisema, iwapo Donald Trump atachaguliwa kuwa rais, angechukua hatua hiyo ya kurarua kadi. 


Add a comment

Choo kithaminiwe, kitunzwe

HIVI karibuni jumuiya ya Kimataifa imeadhimisha Siku ya Choo Duniani kwa lengo la kutoa fursa kwa viongozi, wataalamu wa afya na jamii kujadili juu ya madhara ya kiafya yanayotokana na matumizi duni ya choo. Siku ya Choo Duniani huadhimishwa Novemba 19 kila mwaka na hutumika kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa matumizi ya choo bora. Huhimiza wananchi kujiepusha na magonjwa mbalimbali yanayotokana na matumizi mabaya ya choo.

Add a comment