Dunia inatarajia nini kwa Donald Trump?

DONALD Trump aliyeshinda uchaguzi wa Marekani uliofanyika Novemba 8 mwaka jana, leo anaapishwa huku watu wengi kuanzia Marekani kwenyewe na nje ya taifa hilo kubwa duniani wakiwa na mtazamo na maoni tofauti. Kuapishwa kwa Trump kuwa rais wa 45 wa nchi hiyo, kunahitimisha miaka minane ya utawala wa rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Afrika, Barack Obama.

Add a comment

Tunakula misuli, hatuli nyama

NYAMA ni kitoweo ambacho kinapendwa na wengi. Jambo muhimu ambalo halifahamiki na walaji wa nyama ni ubora wake. Kutokana na ukosefu wa maarifa ya kutosha katika ubora wa nyama, Halmashauri ya Manispaa ya Songea imeamua kutoa mafunzo maalumu ya ubora wa nyama kwa maofisa mifugo kutoka kata zote 21 za manispaa hiyo.

Add a comment

Changamoto kufundisha Hisabati

KUNA wakati mwalimu wa Hesabu anafanya vitendo fulani darasani anapofundisha lakini vikaleta changamoto kwa wanafunzi. Mwalimu anaweza kubaki kushangaa kwa nini wanafunzi hawaelewi au hawajifunzi baadhi ya dhana za somo la Hisabati. Utafiti umeonesha kuwa changamoto hizi hutokana na jinsi wanafunzi wanavyotafsiri kile wanachosikia na kile walichokizoea katika mazingira yao.

Add a comment