Ziara ya RC ilivyoongeza morari kwa walimu

WALIMU wa shule za msingi na sekondari wilayani Kongwa, mkoani Dodoma wamekongwa nyoyo na mtindo aliotumia Mkuu wa Mkoa huo, Jordan Rugimbana kutafuta ufumbuzi wa kero zao. Kitendo cha Rugimbana kutembelea na kuzungumza nao kwenye shule ya msingi Mnyakongo na sekondari ya Kongwa, kumewapa faraja na imani kwamba anawajali. Katika mazungumzo nao, amebaini namna gani anaona hawana furaha na akaweka mkakati wa kupanga safari kuzungumza nao kiundani kero zao.

Add a comment

Hotuba ya Obama haina ujumbe Afrika?

RAIS wa Marekani anayemaliza muda wake Ijumaa, Barack Obama, wiki iliyopita alitoa moja ya hotuba zake za kuaga ambapo alisisitiza haja ya Wamarekani kuungana. Akizungumzia hali ya taifa hilo kubwa anayoiacha, Obama alizungumzia pia namna uchumi wa Marekani ulivyoimarika lakini pia akazungumzia tishio la kundi linalojiita Dola la Kiislamu (IS).

Add a comment