Mbao yazionya Yanga na Azam

Uongozi wa timu ya soka ya Mbao FC umeahidi ushindi kwa michezo yake mitatu iliyobakia. Mbao FC imebakiza mechi dhidi ya Azam FC,Yanga na Kagera Sugar. Akizungumza na gazeti hili Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Soud Slim alisema timu yao imejipanga vyema kwajili ya kuhakikisha inazifunga timu hizo ili kuhakikisha inabakia katika ligi kuu.

Add a comment