Lampard astaafu soka

Kiungo wa zamani wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya soka ya Uingereza Frank Lampard amestaafu soka baada ya kipindi cha miaka 21 ya kupiga kabumbu.

Lampard mwenye umri wa miaka 38 amekuwa akiichezea klabu ya New York City katika ligi kuu ya Marekani maarufu kama Major League Soccer.

"Wakati nimepokea ofa nzuri za kuendelea kucheza, katika umri wa miaka 38 nahisi sasa ni wakati kuanza maisha mpya, alisema Lampard.

Amecheza mechi 649 akiwa Chelsea na mara 106 katika timu ya taifa.

"Nakishukuru chama cha soka kwa kunipa nafasi kusomea ukocha na ni matarajio yangu nitatumia nafasi zitakazopatikana nje ya uwanja," alisema.

 

Add a comment