Simba karata ya mwisho

SIMBA leo ina kazi nyingine ngumu itakaposhuka kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam kumenyana na Stand United katika mechi ya Ligi Kuu Bara. Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kulingana na mahitaji ya timu zote mbili na Simba ikipoteza maana yake inajiondoa kwenye mbio za ubingwa, hivyo hiyo ni karata yake ya mwisho.

Add a comment

…Wakishinda tumekwisha - Omog

KOCHA Joseph Omog wa Simba amesema kama mahasimu wao Yanga wataendelea kushinda mechi zao basi suala la ubingwa kwao litakuwa gumu. Simba inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 62 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 59 lakini ni Yanga ndio iliyo kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa kama itazitumia vizuri mechi hizo.

Add a comment