Matumla Jr aruhusiwa hospitali

BONDIA Mohamed Matumla Jr (30) ambaye alifanyiwa upasuaji wa kichwa hivi karibuni, ameruhusiwa jana kurudi nyumbani. Msemaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (MOI), Jezza Waziri alisema jana kuwa madaktari wamejiridhisha na afya ya bondia hiyo na kuamua kumruhusu huku wakifuatilia maendeleo yake kwa karibu.

Add a comment