Na wanaume wanaolewa!
- Imeandikwa tarehe 01 Juni 2012
- By Basil Msongo
- Imesomwa mara: 1741
SEMA mtu wangu, bila shaka mambo ‘mzuka’ au vipi, pole kwa majukumu na starehe za hapa na pale. Namshukuru Mungu sijambo, mambo yanakwenda, wanabana lakini ni muhimu kuwa king’ang’anizi , ‘laifu iz not lelemama’, na usisahau kwamba, mtaji wa masikini ni nguvu zake.
Usipende kubebwa, usiendekeze mbeleko, tumia juhudi kwa kila unalofanya ili kuishawishi jamii ikukubali, inawezekana, timiza wajibu wako.
Kuna vijana wa kiume wanaopenda vya dezo a.k.a kitonga, hadi wameamua kubadili asili ya uumbaji, na wengine wameolewa na wanaume wenzao!
Jamii inaweza kuona kuwa ni jambo dogo lakini litakuwa na madhara makubwa baadaye, mtoto aliyezaliwa leo akifika umri wangu hali ya ushoga itakuwaje nchini?
Tusiruhusu mambo ya kijinga yanayotokea kwa wazungu yawe mambo ya kawaida kwa Watanzania. Vijana mashoga wapo wengi tu tunapoishi, wanafahamika, tunaishi nao, tunakula nao, tunakunywa nao, tunastarehe nao, na hata mimi nawafahamu, na hawaoni ubaya wa wanayoyafanya.
Lakini ukiangalia upande wa pili wa shilingi ni wazi kwamba, mashoga wapo kwa kuwa kuna wanaohitaji hiyo ‘huduma’ wanayotoa, na hata wasagaji wapo kwa kuwa wana ‘mademu’ wao.
Hivi sasa nchi nyingi zinajadili ndoa za mashoga, Rais wa Marekani, Barack Obama anasema si jambo baya, na wabunge wa Australia wamegawanyika, kuna wanaopinga, na wengine wanataka sheria ya ndoa ibadilishwe ili wanaume waruhusiwe kuoana.
Ndoa za mashoga zikihalalishwa, wanawake wasagaji nao watataka jamii iwatambue na waruhusiwe kuoana.
Vijana tuna jukumu la kuhakikisha kwamba, jamii haioni kwamba, ushoga ni jambo la kawaida, kwa kuwa kasi ya ongezeko la mashoga mitaani linanishawishi niamini kwamba, ipo siku, wataanzisha chama chao, Chama Cha Mashoga Tanzania (CMT).
Wataenda kwa Msajili wa Vyama kuomba kusajiliwa, wakikataliwa wataandamana kudai haki yao kwa kuwa wapo wengi na jamii inawatambua, na ipo siku wataomba wawe na mwakilishi wao bungeni (Mbunge wa Viti Maalumu - Mashoga).
Mashoga Tanzania wameamua kuwa wazi pengine kwa sababu hata wenzao huko nje hawajifichi, na hali ikiendelea hivi jamii itawazoea, idadi yao inaongezeka na huenda itazidi kuongezeka.
Watakapopata ‘uhalali’ kwenye mtazamo wa jamii, wataunganisha nguvu na wasagaji ili pia wawe na nguvu kiuchumi pengine kupitia Saccos yao (Chama Cha kuweka na Kukopa Cha Mashoga na Wasagaji). Siku njema.
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.


