Ziara ya Rais Museveni imeleta manufaa mengi

RAIS Yoweri Museveni wa Uganda amemaliza ziara yake ya siku mbili ya kikazi nchini na kurejea kwake. Yapo mambo mengi yenye manufaa, ambayo Rais Museveni alizungumza na kukubaliana na mwenyeji wake, Rais John Magufuli katika ziara yake hiyo, ikiwemo ujenzi wa bomba la mafuta, lenye urefu wa kilomita 1,443 kutoka Hoima, Uganda hadi Bandari ya Tanga. Linajengwa na Kampuni ya Total.

Add a comment