loader
Picha

Tamwa yahimiza ulinzi haki za mtoto

CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa) kimeungana na mashirika mengine yanayotetea haki za binadamu na kupinga ukatili wa kijinsia nchini kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika.

Siku hiyo, iliadhimishwa rasmi jana na jijini Dar es Salaam, iliadhimishwa katika Wilaya ya Ilala, kata ya Kivule na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya, Sophia Mjema. Kaulimbiu mwaka huu ni ‘Kuelekea Uchumi wa Viwanda, Tusimwache Mtoto Nyuma'.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa, Edda Sanga, kaulimbiu hiyo inamlenga kila mzazi, mlezi, ndugu, jamaa, jirani na rafiki kumpenda mtoto kwa kuhakikisha anatunzwa vizuri na haki zake zinalindwa ipasavyo ili atimize ndoto zake.

“Takwimu za Shirika la Hali ya Afya na Uzazi (TDHS) mwaka 2015/16 zinaonesha idadi ya wasichana wanaopata watoto katika umri wa miaka 15 hadi 19 imeongezeka mpaka kufikia asilimia 27 mwaka 2015 kutoka asilimia 23 mwaka 2010, hali ambayo inaonesha watoto hawa wanaopaswa kuwa shule badala yake wamepata watoto wakiwa na umri mdogo wakakatisha masomo,” alisema.

Kwa mujibu wa Sanga, utafiti uliofanywa na Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (Unicef) wa mwaka 2015, Tanzania ina asilimia 3.5 ya watoto wenye umri wa miaka saba hadi 17 walio nje ya shule.

Hii inajumuisha watoto takriban milioni mbili waliotakiwa kuwa shule za msingi na watoto takriban milioni 1.5 waliotakiwa kuwa shule za sekondari.

Alifafanua kuwa katika takwimu za Jeshi la polisi nchini kupitia kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz mwaka jana, zinaonesha makosa ya ubakaji na kunajisi yameongezeka kutoka 6,985 yaliyoripotiwa mwaka 2016 mpaka makosa 7,460 mwaka jana.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi