107 mbaroni kwa makosa mbalimbali

TANGA: JESHI la Polisi mkoani Tanga, limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 107 kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya mauaji,wizi wa mifugo,unyang’anyi wa kutumia silaha ,kuingia nchini bila kibali pamoja na kupatikana na dawa za kulevya aina mbalimbali.

Hayo yalisemwa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Almachius Mchunguzi wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu oparesheni zilizofanyika kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Oktoba hadi Novemba 27, 2023.

Kamanda Mchunguzi amesema  kati ya watuhumiwa hao 21 wamekamatwa na Bangi kilogramu 43, Mirungi Kilogramu 124, Heroin Gramu 242 huku wanne  wakikamatwa kwa kosa la kusafirisha wahamiaji haramu na watuhumiwa saba  raia wa Ethiopia kuingia nchini bila kibali.

Aliwataja wengine ni mtuhumiwa mmoja kupatikana na kosa la unyang’anyi kwa kutumia silaha aina ya Panga na watuhumiwa wengine 74 wamekamatwa huku upelelezi ukiwa bado unaendelea.

Aidha Kamanda Mchunguzi amesema pia katika kuimarisha doria za nchi kavu na baharini Novemba 21 mwaka huu huko maeneo ya Kisiwa cha Jambe Wilaya ya Tanga walifanikiwa kukamata boti aina ya Fibre yenye rangi nyeupe na bluu isiyokuwa na usajili ikiwa na injini ya Yamaha HP 15.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button