11 wadakwa gesti wakiwa nchini kinyemela

11 wadakwa gesti wakiwa nchini kinyemela

RAIA 11 wa Somalia wakiwamo watoto watatu wa kike wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuingia nchini bila kibali baada ya kukutwa katika nyumba ya kulala wageni jijini Mbeya.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga alisema watu hao walikamatwa Machi 27 mwaka huu katika msako unaoendelea mkoani Mbeya.

Watoto wawili wana umri wa miaka minane kila mmoja na mwingine ana umri wa miaka 15. Pamoja na watu wazima tisa.

Advertisement

Walikutwa katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Rubi iliyopo wilayani Kyela mkoani hapa wakijiandaa kwenda Malawi.

Aliwataja waliokamatwa ni Ibrahim Hussein Muhamed (42), Abdikafi Hassan (26), Ramadhan Taju (26), Muhamed Nuria (26), Abdirahman Ally (27), Faud Jimale (19), Abdulrahman Samari (20) na Hanad Muhamed (22).

 

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *