238 wanaswa maandamano Kenya

JESHI la polisi nchini Kenya linawashikilia waandamanaji 238 walioandamana jana katika mji wa Kisumu nchini Kenya wakipinga kupanda kwa gharama za maisha.

Taarifa iliyotolewa leo Machi 21, 2023 na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Japhet Koome imeeleza watu wanne kati ya hao ni viongozi wa Azimio na kwamba waliachiwa jana jioni na wanatarajia kupelekwa mahakamani Alhamisi.

Advertisement

“Tungependa kuujulisha umma kwamba wakati wa maandamano Jumatatu, tulikamata watu 25, huku maafisa saba wakijeruhiwa Nyanza; huku Nairobi, magari 10 ya polisi yaliharibiwa, maafisa 24 walijeruhiwa huku watu waliokamatwa wakiwa 213”.alisema Japhet Koome.

IGP Koome alilaani machafuko hayo ambayo aliyataja kuwa “haramu” na kuwapongeza maafisa wake kwa “kuzuia maandamano hayo.

“Kwa hivyo tunalaani kwa nguvu zote, ghasia zisizo na msingi ambazo zilitekelezwa dhidi ya maafisa wetu wanaotekeleza majukumu yao rasmi,” alisema.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *