KURUGENZI ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imewatahadharisha watanzania juu ya utapeli unaofanywa na baadhi ya watu kwa kuwapa email inayosomeka zuhuruyunus250@gmail.com ili kupata teuzi mbalimbali za rais.
Taarifa iliyotolewa leo Aprili 6, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhuru Yunus imeeleza kuwa watu hao kupitia barua pepe hiyo wamekuwa wakiomba kutumiwa pesa ili wapate teuzi katika taasisi mbalimbali serikalini.
Aidha, taarifa ya ikulu imeeleza kuwa ofisi hiyo haihusiki na barua pepe hiyo, na kuwataka watanzania kuepuka utapeli dhidi ya watu hao.
Comments are closed.