Shughuli za kibinadamu hazijadhibitiwa mradi wa JNHPP

RIPOTI Kuu ya Ukaguzi katika Miradi ya Maendeleo ya Mwaka 2022 iliyochapishwa wiki hii imeonesha kumekuwepo na shughuli za kibinadamu zisizodhibitiwa katika sehemu ya juu ya mradi wa kufua umeme wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) katika eneo la juu ya mto kunahatarisha uhaba wa maji kutokana na matumizi haramu ya maji.

Mkaguzi Mkuu wa Serikali amesema vyanzo vya maji visivyolindwa, miundombinu mibovu ya umwagiliaji, kilimo cha biashara, mashamba makubwa, malisho ya mifugo na maendeleo ya makazi ya watu mijini inaweza athiri mradi huo unapangwa kuzalisha megawati 2115 za umme.

“Kuna mifereji ya umwagiliaji isiyo sakafiwa inayopoteza maji kwa njia ya udongo na uvamizi wa mito ulisababisha uharibifu na kujaa kwa udongo ndani ya mita 60 na hivyo kusababisha ufinyu wa eneo la mto,” imesema ripoti ya CAG.

Advertisement

Amesema ufugaji haramu wa mifugo na ukataji miti kwa ajili ya kilimo na uchomaji mkaa karibu na vyanzo vya maji katika Bonde la Kilombero umeongezeka.

Pia “nimebaini kuwa shughuli za kibinadamu zimesababisha kupungua kwa eneo lililotengwa la mto Kilombero eneo la Bonde la Ramsar – Kilombero na limepungua kutoka kilometa za mraba 7,950 hadi 2,193 sawa na asilimia 72 ndani ya miaka 20 tu, na kusababisha upotevu mkubwa wa maji