Yanga yatinga Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Afrika

KLABU ya Yanga kutoka Tanzania, kwa mara ya kwanza imefuzu nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kuiondoa timu ya Rivers United kutoka Nigeria.
Yanga imeingia nusu fainali baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 katika michezo miwili ya nyumbani na ugenini.

Yanga itacheza na Marumo Gallants F.C. ya Afrika Kusini katika mchezo wao wa nusu fainali, ambayo pia itakuwa na michezo miwili nyumbani na ugenini.
Marumo Gallants F.C. imeingia nusu fainali baada ya kuiondosha Pyramids ya nchini Misri kwa mabao 2-1 katika michezo yote miwili ya nyumbani na ugenini.
Aidha, timu ya Asec Mimosas ya Ivory Coast imefuzu nusu fainali ya michuano hiyo, baada ya ushindi wa mabao 2-0, na sasa itasubiri mshindi kati ya USM Alger na As Far Rabat mchezo wa leo saa 4 usiku.

Habari Zifananazo

Back to top button