ARSENAL imeongeza dau hadi kufikia pauni milioni 60 wakitaka huduma ya kiungo Kai Havertz kutoka Chelsea.
Mjerumani huyo ameonesha nia ya kusepa Chelsea hata hivyo bado klabu yake haijathibitisha kukubaliana na dau hilo.
Havertz alijiunga na Chelsea 2020 kwa dau la pauni milioni 85 na kusaini mkataba wa miaka mitano.
Mpaka sasa mkataba wa nyota huyo umebaki miaka miwili hata hivyo hana nia ya kuendelea kucheza klabuni hapo.