Uwanja wa Karume kuvunjwa

KATIBU Mkuu,  Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Said Yakubu amesema uwanja wa Karume Dar es Salaam unatarajiwa kuvunjwa kupisha maboresho ambapo pia kutajengwa hoteli ya kisasa.

Kauli hiyo ameitoa katika maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ‘Sabasaba 2023’ alipotembelea banda la Wizara yake ikiwa ni maonesho ya kwanza ya Wizara hiyo tangu ijitegemee.

“Leo hii nimekuwa na mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia amenionesha mipango yao na namna wanavyoshirikiana na sekta binafsi.” Amesema.

Advertisement

Amesema, Karia amemueleza uwanja wa Karume utavunjwa na kujengwa mwingine pia ujenzi wa hoteli kwa ushirikiano wa TFF na sekta binafsi.

Aidha, Yakub amesema, katika mradi huo kutakuwa na fursa za ajira katika kipindi chote cha ujenzi na hata utakapo kamilika.

Kwa upande mwingine, amesema serikali imeomba kushiriki kuandaa michuano ya mataifa Afrika AFCON mwaka 2027 huku ikihusisha ushirikiano wa sekta binafsi.

 

1 comments

Comments are closed.