‘Rais Samia, Dk Mpango watafanya ziara Kusini’

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

RAIS Dk Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Rais Dk Philip Mpango, wanatarajia kufanya ziara katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kwa ajili ya kukagua miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hayo leo mkoani hapa, wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ligula, mkoani Mtwara.

“Nawajua mlikuwa mnalalamika kwamba viongozi hawafiki , Mkoa huu (Mtwara)  ni mkoa wa kimkakati, kuna wakati tunaambiwa  simama kidogo, sasa nenda, sasa wamesema tuje,” amesema.

Advertisement

Amesema Rais atakuja na Makamu wa Rais watakuja wakianzia katika Mkoa wa Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Amewataka wabunge na viongozi wengine kujipanga kwa kuhamasisha wananchi kujitokeza wakati wa ziara ya viongozi hao wa kitaifa.

Majaliwa amesema yeye ametangulia kusafisha njia ili Rais na Makamu wa Rais waweze kufanya ziara yao.

 

4 comments

Comments are closed.

/* */