Dirisha la usajili lipo kwa Simba, Yanga na Azam pekee?

WIKI moja imepita tangu dirisha la usajili kwa timu za madaraja ya Ligi Kuu, Championship, Daraja la Kwanza na Ligi Kuu ya Wanawake lifunguliwe. Kufunguliwa kwa dirisha hilo kunatoa nafasi kwa viongozi wa timu zote zilizo kwenye madaraja hayo kusajili wachezaji kuimarisha vikosi vyao. Lengo kubwa la Caf na Fifa kuweka dirisha la usajili ni kutaka kuwepo na ushindani wakweli kwenye ligi ya nchi husika.

Achana na masuala ya uwezo wa kifedha ambalo limekuwa tatizo kubwa kwa timu nyingi za Tanzania lakini siku za karibuni jambo hilo nikama linaelekea kuisha. Lakini tangu dirisha hilo lifunguliwe ni timu tatu hadi nne ndizo zinazoonekana kuwa bize katika mchakato huo wa kuimarisha vikosi vyao.

Kila kunapokucha utasikia Yanga, Simba na Azam wamemtambulisha mchezaji fulani hawa wamemalizana na yule hizo timu nyingine 13 ni kama hazihusiki na dirisha.

Advertisement

Maswali yakujiuliza ni mengi kwamba ukimya wao ndio tuseme hawana fedha za kufanya usajili au vikosi vyao vya msimu uliopita bado vina uwezo wa kufukuzia ubingwa msimu ujao? Jibu siyo kweli isipokuwa viongozi wa timu hizi tayari wameka- ta tamaa na wamekubali kwamba ligi hii ni ya timu tatu za Simba, Yanga na Azam.

Viongozi wa timu hizi ndio wamekuwa mstari wa mbele kutupa lawama kwa waamuzi kwamba wanazipendelea timu hizo tatu.

Wakitoka kwa waamuzi watahamishia lawama zao kwa wachezaji kwamba wameuza mechi na mambo mengine kama hayo. Sababu ya ligi yetu kupewa hadhi yakuwa namba tano Afrika ni ushindani uliopo lakini zipo baadhi ya timu kama hazijitambui kwamba zipo katika ligi gani.

Leo tunaambiwa baadhi ya timu zimeshakamilisha usajili wao na hata kuzindua jezi zao za msimu ujao lakini wao wapo kimya. Viongozi wa klabu nyingi ndogo ni kama hawajui wajibu wao katika kuzitumikia nafasi walizoomba kuzitumikia katika timu hizo.

Inawezekana timu hizo zinafanya usajili kimya kimya bila kujinadi kama ilivyo kwa klabu hizo kubwa lakini usiri wa nini wakati taratibu zenyewe za usajili zipo wazi? Kuna haja viongozi wa timu hizi ndogo wakatambua ukubwa wa nafasi walizonazo na matokeo mazuri sababu pindi matokeo yanapokuwa mabaya sababu zinakuwa nyingi kwa TFF na waamuzi

5 comments

Comments are closed.