Ahukumiwa miaka 60 kwa kumbaka mwanafunzi

MAHAKAMA ya Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani Imemhukumu Alexander Charles Ndogole (53) kifungo cha miaka 60 jela kwa kosa la kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi wa shule ya sekondari Visiga.

Akisoma hukumu hiyo, leo julai 11,2023 mahakamani hapo, Hakimu Mkazi, Mahakama ya Wilaya ya Kibaha, Felister Ng’hwelo alisema Ndogole alitenda kosa hilo mwezi Februari mwaka 2023, Visiga, mjini Kibaha.

Hakimu huyo Ng’hwelo, alisema mahakama hiyo imeridhishwa na ushahidi usiokuwa na shaka kwamba mshitakiwa alitenda kosa hilo Kwa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 14 ambaye alikuwa ni baba wa kufikia.

“Mahakama imemtia hatiani mshitakiwa Kwa kosa la kwanza la kubaka chini vifungu vya sheria 130, kifungu kidogo cha kwanza na cha pili, e, cha sheria ya makosa ya jinai sura ya 16 na kosa la pili la kumpa mimba kifungu cha 60 A, kifungu kidogo cha tatu cha sheria ya elimu hivyo kosa la kwanza miaka 30 na kosa la pili miaka 30.”ameeleza hakimu huyo.

Amesema mahakama imeridhishwa na ushahidi uiotolewa na mwanafunzi huyo ambapo alieleza bayana kwamba walikuwa wakiishi nyumba moja na mshitakiwa kutokana na kwamba alikuwa ni baba yake wa kufikia ambapo alitumia mwanya huo kumbaka na kumpa mimba.

“Kesi hii namba 27 ya mwaka 2023 imepata ushahidi wote muhimu na mtoto alieleza mazingira halisi mshitakiwa alivyokuwa akifanya maana alikuwa ni baba wa jambo.

“ameeleza

Awali akitoa utetetzi mahakama hapo Mshitakiwa huyo, aliiomba huruma ya mahakama baada ya kueleza alitenda kosa hilo kutokana na ugomvi alikuwa nao na mke wake ambaye ndiye mama mzazi wa mtoto huyo.

Pamoja na utetezi huo mahakama hiyo ilitupilia mbali hoja hiyo na kumtia hatiani huku ikieleza kwamba mshitakiwa hakuwa na kielelezo chochote kilichonyesha kwamba mwanafunzi huyo namna alivyokuwa akihusika na ugomvi wa wawili hao.

Habari Zifananazo

Back to top button