BEKI wa zamani wa Manchester City, Benjamin Mendy amekutwa hana hatia ya katika mashitaka mawili yaliyokuwa yakimkabili moja la ubakaji na lingine la kujaribu kubaka.
Maamuzi hayo yalipotolewa na msimamizi wa Mahakama ya Chester Crown Kaskazini Magharibi mwa Uingereza leo.
Mfaransa huyo alikutwa hana hatia ya makosa sita ya ubakaji na moja la unyanyasaji wa kingono dhidi ya wasichana wanne ambapo alibakiwa na makosa mawili ya kubaka na kujaribu kubaka ambayo leo yamefutwa yote.
Mendy alijiunga na Manchester City 2017 akitokea AS Monaco.