30,000 waajiriwa Geita miaka 3 ya Samia

GEITA: Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kutoa fursa za ajira, ambapo kwa Mkoa wa Geita zaidi ya wafanyakazi 30,000 wapya wameajiriwa katika kipindi cha miaka mitatu.
Shigela amesema hayo leo katika sherehe za Mei Mosi, ambapo kwa Geita yalifanyika wilayani Mbogwe na kueleza kuwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 Wilaya ya Mbogwe pekee imepokea watumishi wapya zaidi ya100.
Amesema, ndani ya miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan, amejenga zaidi ya madarasa 3000 na kusisitiza kuwa wafanyakazi katika mkoa wa Geita ni watu muhimu na kazi wanazofanya zinathaminika.
Amewataka waajiri wa sekta binafsi na sekta ya umma wasiwazuie wafanyakazi wao kushiriki sherehe za Mei Mosi, kwani wafanyakazi wana haki ya kukutana na kubadilishana uzoefu na wenzao wa maeneo tofauti tofauti.