Pinda asherehekea miaka 75 ya kuzaliwa Mtwara

WAZIRI Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda leo ameadhimisha miaka 75 ya kuzaliwa kwake mkoani Mtwara.

Maadhimisho hayo yameanza na sala takatifu iliyofanyika majira ya saa 4 asubuhi katika Kanisa Kuu la Watakatifu Mtwara sambamba na kuunga mkono kwa vitendo jitihada za mfuko wa kiuchangiaji wa elimu mkoani humo (MPEF) kwenye jitihada ya kutafuta fedha kwa ajili ya ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wenye uhitaji.

Mfuko huo ulizinduliwa rasmi Januari 2021 ukiwa ni wazo la pamoja kati ya mkoa huo na jimbo Katoliki Mkoa wa Mtwara na Chuo Kikuu cha Saut (Stemco) wenye lengo la kuunga mkono jitihada za serikali katika kuhakikisha hakuna mtoto, kijana wa kitanzania anayeachwa nje ya fursa za kujiendeleza kielimu kutokana na changamoto hiyo.

“Tukio hili ni la kipekee na safari ya miaka 75 ni ndefu katika maisha ya binadamu hivyo tuna kila sababu ya shukuru kwasababu ni jambo la kiroho na ni maisha ya kawaida.” amesema Pinda.

Aidha kuhusu mfuko huo ameridhishwa na kuupenda kwani ukasaidie wengine ambao wana uhitaji huo huku akisisitiza kwamba mfuko uendelee badala ya kurudi nyuma.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amempongeza Waziri Mstaafu huyo kwa kuona umuhimu wa jambo hilo na kuja kuchangia juhudi hizo kwa kuendesha harambee ya kutunisha mfuko huo ili aweze kuwafikia wanafunzi wengi zaidi.

“Haya ameyafanya mengi katika taifa hili kwa nafasi yake ya uongozi bado anaendelea kuifanya kazi hii ambayo ina baraka nyingi zaidi za Mungu kuliko utumishi wa kiserikali aliuopata”,amesema Abbas

Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko huo Padre Alex Masangu amesema mfuko huo umekuwa muhimu kwa kuchangia masomo kwa wanafunzi wenye changamoto hiyo kwani mpaka sasa idadi ya wanafunzi waliyofadhiliwa kwa mwaka wa kitaaluma 2021/22 ni 1064 na mwaka 2022/23 wanafunzi 1128 kutoka mikoa yote 26 tanzania Bara.

Habari Zifananazo

Back to top button