Vanilla International wafungua mradi Kenya

KAMPUNI ya Vanilla International Limited ya Tanzania, imefungua mradi wa Vanilla Village nchini Kenya, eneo la Mombasa mji mdogo wa Mariaani, baada ya kupokea maombi mengi kutoka nchini humo.

Mradi huo umefunguliwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Simon Mnkondya, ambapo aliwapongeza wananchi wa Kenya kwa kutambua utajiri uliojificha katika uwekezaji huo, hivyo kutaka kuwekeza.

Mnkondya alisema amefanya uamuzi huo, baada ya Wakenya wengi kuonesha uhitaji mkubwa wakuwekeza katika kilimo cha vanilla na kuvutiwa na mradi wa Tanzania, ambao una mashamba katika maeneo ya Arusha, Zanzibar na Dodoma.

Mnkondya amewataka Wakenya kujitokeza zaidi kuwekeza katika kilimo cha vanilla kwa mfumo wa mashamba Shufwaa yaani block Farming, kupunguza gharama za uwekezaji, kwa ajili ya usalama na kwa ajili ya kuhakikisha uwepo wa soko la vanilla.

Naye Dipan Shah Mkurugenzi wa Nyali Cinemax amesema Vanilla India imewafanya wakulima wawe matajiri sana kwa maana ni zao la pili kwa bei duniani.

Kauli kama hiyo pia ilizungumzwa na Bruno Cern’o Rais wa Upendo Foundation, ambaye ana asili ya Italia amesema kwa vile vanilla ni zao la bei kubwa ni vyema sasa Waafrika kulima vanilla ili kupata utajiri endelevu na kuwa na unafuu wa maisha.

Amesema lengo la mradi wa Vanilla Village Kenya ni kukuza uchumi wa wananchi na Waafrika kwa ujumla.

Habari Zifananazo

Back to top button