CHAMA cha Wahasibu Wanawake Tanzania (TAWCA) kimeagizwa kuendelea na mipango mbalimbali ya kwa ajili ya kuongeza wanawake wengi zaidi katika fani ya uhasibu hapa nchini.
Ombi hilo limetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Dk Angelina Mabula wakati uzinduzi wa mkutano wa sita wa chama hicho uliofunguliwa leo wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Dk Mabula amewapongeza TAWCA kwa mipango mbalimbali katika kuongeza wahasibu wanawake nchini. Amewataka wahasibu Wanawake kutumia siku mbili za kongamano hilo la kuweza kujifunza mambo mbali ya uhasibu.
Amewaagiza wahasibu hao kutumia taaluma zao kwajili ya kuweza kuleta maendeleo mbalimbali katika jamii.
Ametoa rai kwa TAWCA kuendelea kuongeza ushawishi kwa wanawake nchini kusomea fani ya uhasibu pamoja na kujiunga katika chama cha TAWCA.
Dk Mabula ameipongeza TAWCA kwa kuweza kusaidia wanawake 101 kuweza kupata Elimu ya fedha katika mkoa wa Dar-es-salaam.
Amesema Rais Samia Suluhu ameweza kuongeza nafasi ya viongozi wanawake nchini na sasa ni asilimia 40 ya wanawake wapo katika nafasi za juu za uongozi.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Tanzania(TAWCA) Dk CPA Neema Kiure amesema mpaka sasa chama chao kimefanikiwa kuwasajili wahasibu wanawake 920 katika chama chao.
Amesema chama chao kimefanikiwa kutoa elimu ya fedha kwa wanawake 101 katika mkoa wa Dar-es-salaam.
‘’Tumekuwa wadau wakubwa sana katika kununua vitabu vya hisabati katika shule mbali mbali hapa nchini zikiwemo Turiani na Kurumula.’’ Amesema Dk CPA Kiure.
Ameahidi wataendelea kuandaa makongamano mbali mbali ya kuweza kuwasaidia wanawake wahasibu katika jamii.
‘’Tuna mpango malumu wa kusaidia wanawake mbali mbali kuweza kujieleza na kuwafundisha jinsi ya kuandaa CV zao wakati wa kuomba ajira’’ amesema Dk CPA Kiure.
Amesema kwa sasa wapo katika mpango wa kujenga jengo la TAWCA katika mkoa wa Dodoma na tayari wameshanunua kiwanja kwajili ya ujenzi huo.