Korosho kusafirishwa Bandari ya Mtwara

WAKUU wa mikoa ya Mtwara, Ruvuma na Lindi wamekubaliana kusafirisha korosho ghafi kwa kutumia Bandari ya Mtwara kwenye msimu wa zao hilo utafunguliwa Oktober, 21 mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa Lindi, Zainab Terack amesema hayo leo wakati alipozungumza na wajumbe wa kikao cha tathmini zao la mbaazi, ufuta na maandalizi ya msimu wa zao la korosho kilichowashirikisha wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, Manispaa ya Lindi, maafisa kilimo, ushirika, taasisi za fedha, vyama vikuu vya ushirika msingi, wakulima na watunza maghala wasagirishaji , kilichofanyika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini hapa.

Amesema kuwa korosho ghafi zote kutoka mikoa ya Lindi na Ruvuma ziletwe katika Bandari ya Mtwara tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi kwa kutumia meli.

Amesema kuwa wasafirishaji wote wanatakiwa watoe malori yao badala kupeleka mkoani Dar es Salaam msimu huu wapeleke Mtwara.

Hata hivyo wadau wa kikao hicho kwa nyakati tofauti walidai kuwa bandari hiyo kuna changamoto za makontena ya uhifadhi korosho yako machache, pia kuna ucheleweshaji wa kupokea korosho.

Aidha gharama za uhifadhi katika makontena ni kubwa ukilinganisha na Bandari ya Dar es Salaam kuna maeneo mengi ya uhifadhi na kurudi kuchukua korosho zingine ghafi.

Walidai kuwa kama changamoto hizo hazijatolewa itasababisha mkulima kupata bei ya chini.

Kwani gharama za usafirishaji zitakuwa kubwa na foleni nayo itakuwa kubwa kwa hiyo ununuzi nao utasuasua

Zaidi ya kilo 78,620,000 zinatarajia kukusanywa korosho ghafi na kuuzwa kwenye msimu wa mwaka huu.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
5
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x