Maonesho biashara Afrika Mashariki yazinduliwa leo

MAONESHO ya 24 ya Biashara ya AfriKa Mashariki ya kuonesha bidhaa mbalimbali ambazo zinazalishwa ndani ya nchi na nje ya nchi yamefunguliwa rasimi leo.

Takribani ya kampuni 120 zitashiriki maonesho ya bidhaa ikiwa kampuni 25 ni za Kitanzania na kampuni 95 kutoka mataifa ya Afrika Mashariki, Ulaya na Asia.

Akizungumza wakati akifungua maonesho hayo, Waziri wa Viwanda na Biashara Dk.

Ashatu Kijaji amesema zinapokutanishwa kampuni hizo kuonesha bidhaa zao nchini kunaleta fursa ya kuongeza ajira na kuzipa thamani malighafi zinazozalishwa hapa nchini na kutengeneza bidhaa halisi.

Aidha amesema maonyesho hayo yanasaidia sana katika kuongeza uwekezaji kutokana na wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali kutumia fursa ya maonesha kubuni bidhaa zenye uwezo wa kuzalishwa Tanzania na kuanzisha viwanda.

Ameongeza kuwa uwekazaji kwa sasa umeongezeka hususani wa viwanda kutokana na kuongezeka kwa viwanda vingi huku akitoa wito kwa watanzania kushiriki maonesho hayo na kujipatia fursa mbalimbali.

Mkurugenzi Mkuu wa Biashara Afrika Mashariki Expo group Duncan Njage amewasihi Watanzania kuja kujitokeza kuona bidha bora katika maonesho kwani mbali na kuleta fursa yatawapatia ajira ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Maonyesho hayo yatadumu ndani ya siku 3 kuanzia leo oktoba 19 hadi 21.

Habari Zifananazo

Back to top button