Dar es Salaam kujengwa hospitali ya Apollo

TANZANIA na Mtandao wa Hospitali za Apollo kutoka India zimeingia makubaliano ya kudumu ujenzi wa hospitali ya Apollo katika jiji la Dar es Salaam lengo ni kutoa huduma za afya zenye ubora na unaozingatia zaidi teknolojia.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dk John Jingu amesema hospitali hiyo itajengwa ndani ya miaka mitatu na itakuwa ya kisasa yenye uwekezaji uliozingatia teknolojia ya juu.

Akitaja faida za uwekezaji huo, DK Jingu amesema licha ya kusaidia huduma bora za afya, lakini pia itasaidia kupunguza gharama na fedha za kigeni kwa wagonjwa ambao wanalazimika kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Dk Jingu amegusia suala la ajira na mafunzo ambapo amesema baadhi ya Watanzania watapata ajira kupitia uwekezaji huo, hata hivyo baadhi ya wataalamu wa afya watapata mafunzo kuhusu huduma za afya.

“Watapata ujuzi wa kisasa, uzoefu kuendana na dunia ilivyo, lakini katika maeneo ya mafunzo yatakuwa kwenye mifupa, kansa kwahiyo watapata pia uzoefu wa namna nzuri ya kuendesha huduma.” Amesema Dk Jingu.

Habari Zifananazo

Back to top button