Wanamitindo watakiwa kuongeza ubunifu

WABUNIFU wa mitindo nchini watakiwa kuongeza ubunifu wa kazi zao ili kutangaza masoko yao na kujitangaza katika soko la Kimataifa.

Akizungumzia na habari leo wakati wa uzinduzi wa darasa la ushonaji kwa wabunifu lililoandaliwa na muandaaji wa Starting Tailoring Bussness with Agusta Masaki amesema Basata inatambua mchango unaotolewa na tasnia ya ubunifu nchini hivyo wabunifu wanapaswa kujituma.

Amesema kuanzishwa kwa darasa hilo ni msaada mkubwa kwa wabunifu wanaotaka kujifunza na kujiendeleza na
darasa la ushonaji kupitia cherehani.

“Zamani kushona ilikuwa nikazi ya kudharaulika tofauti na kipindi hiki ni ajira watu wanajiajiri na kutoa ajira kwa wengine, tunapokea wanafunzi kutoka vyuoni wanakuja kujifunza wanaangalia fursa za wao kupata ajira kupitia sanaa ya ubunifu.”

“Ubunifu umekuwa heshima mafundi cherehani kwa sababu watajitahidi kufanya ubunifu mzuri ili bidhaa zao wanazozitengeneza zikashindaniwe katika soko la kimataifa sio kushona na kubuni mishono iweje kumvutia mteja”,amesema Agusta.

Pia ameongeza kuwa Tanzania ipo katika uchumi wa kati watu wake wana fedha na mtu mwenye fedha anapenda kuvaa vizuri hivyo wabunifu waendelee kubuni kwa lengo la kupata fedha na kutangaza masoko yao ndani na nje ya Tanzania.

Habari Zifananazo

Back to top button