ADHA YA MVUA: Mabasi ya shule yakiwa yamekwama katika barabara ya Atlas inayotenganisha mitaa ya Goba na Mivumoni katika wilaya za Ubungo na Kinondoni, Dar es Salaam Ijumaa asubuhi. Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimearibu miundombinu zikiwemo barabara na kuathiri utoaji huduma za kijamii.